Watu Wanaotumia Vibaya Mitandao ya Kijamii Wakae Chonjo

code         No comments


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa siku zao zinahesabika kwani ifikapo 01/09/2015, 


Sheria ya Uhalifu wa Mitandao ambayo imekwisha sainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa sheria kamili na itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.

Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.

katika taarifa aliyoitoa Mhe. Prof. Makame Mbarawa, waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia kuhusu sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kwa waandishi wa habari tarehe 8 mei, 2015

Alisema

“Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hii. Zipo nchi nyingi duniani zilizo na sheria kama hii. Mfano wa nchi hizo ni Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India(IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act), Uganda (Computer Misuse Act, 2010),Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information andCommunication Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse andCybersecurity Act), Mauritius (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi nyinginezo.”

Akitaja baadhi ya makosa

“ Makosa hayo yanajumuisha uhalifu wa mitandao ambapo simu za mkononi, kompyuta au
mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo. Mifano ya makosa
hayo ni pamoja na yafuatayo:
1. Wizi wa fedha kwa njia ya mtandao;
2. Ugaidi unaofanyika kupitia kwenye mitandao;
3. Maudhui potofu yanayosababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili,
4. Uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa unaofanywa kwa makusudi. Kwa mfano
kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Hii imepelekea Serikali na
watoa huduma na wananchi kwa ujumla kupata hasara na kusababisha ukosekanaji wa
huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii.”

Kumekua na hofu kubwa kwa wadau mbalilimbali wa sekta ya Mawasiliano kua huenda sheria hii inaweza kuzuia uhuru wa vyombo vya habari

Alimalizia kwa kusema

“Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano, Waandishi wa Habari, Wana-blogger, na Wananchi kwa ujumla,kama kuna yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii, basi alete maoni hayo hapa Wizarani. Serikali kupitia Wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, itautafakari na kuufanyia kazi kwa kina. Hii haitokuwa sheria ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama umuhimu huo utajitokeza.”




Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.