KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi katika majimbo matano kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.
Majimbo hayo ni Makete,Busega,Ukonga,Rufiji na Kilolo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya alhamisi Agosti 13.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.
Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea Ndugu Nape amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha CC ambapo kesho na kesho kutwa watamaliza na kikao
PICHA MBALIMBALI KATIKA VIKAO VINAVYOENDELEA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Mzee Steven Wassira wakibadilishana mawazo ukumbini
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zakiah Meghji na Dk. Asha-Rose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini
0 comments: