Vuguvugu la Uchaguzi linazidi kuongezeka hasa tunapozidi kukaribia siku za kuanza kampeni.za madiwani ,wabunge na Uraisi.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi sasa ni mda muaafaka wa kuchukua fomu za kuwania nafai ya Uraisi
Usipitwe: Ratiba ya Uchaguzi Mkuu 2015
Tumeshuhudia waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli mheshimiwa Edward Lowasa akisindikiwa na maelfu ya watanzania katika jiji la Dar es salaam. kwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urahisi katika uchaguzi utakao fanyika mwezi wa kumi mwaka huu 2015
Mh. Edward Lowassa akikabidhiwa Fomu ya kuwania Uraisi |
Idadi hiyo ya watu imeandika historia mpya katika siasa za Tanzani .
Wakati hayo yote yanatokea Mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye nae atawania nafasi ya uraisi kupitia chama cha mapinduzi CMM hakua nyuma.
Magufuli ambaye ni waziri wa Ujenzi na Miundombinu akiambatana na Kikwete Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walizindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika mkoa wa Mtwara
Katika ziara hiyo walizindua kivuko cha MV MFANIKIO kilichogharimu shilingi 3.3 bilioni.
pia walizindua barabara ya kilomita 60 kutoka Ndungu-Somanga.
CCM MTWARA WAMWAKIKISHIA USHINDI WA URAISI
Mh. Magufuli ambaye anafahamika kwa utendaji kazi wake makini amehakikishiwa kuungwa mkono na wanagesi katika mbio za kuwania Uraisi
Baadhi ya wanachama wa CCM Mtwara |
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara |
0 comments: