WAKATI kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa hesabu za mwezi uliopita, hali iko kinyume upande wa Kenya ambako bei za bidhaa zimekuwa nafuu katika kipindi hicho kutokana na mfumuko wa bei kushuka.
Kulingana na takwimu za Idara ya Taifa ya Takwimu (NBS) zilizotolewa jijini Dar es Salaam leo, mfumuko wa bei kwa Kenya umekuwa ni asilimia 6.62 kutoka asilimia 7.03 wa mwezi Juni.
Tanzania imelazimika kukabiliana na kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei kwa sababu bei za bidhaa zimepanda kwa mwezi uliokwisha, kutoka kiwango cha asilimia 0.2 kwa mwezi Juni.
Takwimu hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii katika Idara ya Takwimu nchini, Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini. |
Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei za bidhaa umekuwa imara katika kipindi cha mwaka kutoka Julai 2014, kufikia mwezi uliokwisha, ukiwa ni katika kiwango cha asilimia 6.5 ambacho ni pungufu ya asilimia 0.1 kutoka asilimia 6.4 kiwango cha Julai mwaka huu.
Amesema kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwezi uliopita kimeongezeka kwa asilimia 0.4 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 0.2 kwa mwezi Juni mwaka huu.
“Fahirisi ya bei ya huduma mbalimbali zimeongezeka 158.78 kwa mwezi julai kutoka 149.16 mwezi juni na bei za vyakula na vinywaji baridi zimeongezeka kwa asilimia 10.6 kutoka asilimia 10.1 mwezi juni,” amesema.
Akitaja aina ya bidhaa, Kwesigabo amesema kwa zao la mchele mfumuko wa bei umeongezeka kuwa asilimia 27.9 wakati kwa mahindi ni asilimia 2.3 na unga wa muhogo asilimia 9.2 huku nyama ikiwa ni asilimia 4.5, samaki asilimia 12.2 na maharage asilimia 5.9.
Kwesigabo amesema thamani ya shilingi ya Tanzania imeshuka kwa Shilingi 2.98 mwezi uliopita kutoka Shilingi 100 mwezi Septemba mwaka 2010.
0 comments: