UKAWA Wapewa Ruksa Kuzindua Kampeni zao Jangwani Jumamosi Hii

code         No comments

Ruksa Kutumia Uwanja wa jangwani

ya vyama vinavyounda UKAWA ya kukatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na  taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene zimesema kuwa uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.

Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao.

Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.