Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka huu 2015,
Ratiba inaonyesha Tarehe 21 Agosti 2015 ni siku ya Uteuzi wa Wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani.
Tarehe 22 Agosti 2015 hadi 24 Oktoba 2015 ni Kampeni za Uchaguzi.
Tarehe 25 Oktoba 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Jaji (Mst) wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva amewasihi wadau wa Uchaguzi hasa Vyama vya Siasa na Wananchi kufuatilia ratiba hiyo na kuizingatia kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu.
0 comments: