RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka walimu wa shule za sekondari nchini kutoogopa kufundisha wanafunzi wao masomo ya sayansi kwa lugha ya Kiswahili, kwa kuwa inawezekana na wataelewa.
Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa tuzo katika maonesho ya kitafiti na kigunduzi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika kuibua tafiti mbalimbali za kisayansi, lengo likiwa ni kuimarisha taaluma hiyo pamoja na kutoa hamasa ya kusoma masomo ya sayansi.
Maonesho hayo yaliandaliwa na Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST) ambapo wanafunzi kutoka sekondari ya Mzumbe mkoani Morogoro waliibuka washindi wa jumla na kuzawadiwa udhamini wa kusoma masomo ya vyuo vikuu pamoja na kutembelea nchini Ireland.
Katika utafiti wao, wanafunzi hao walieleza jinsi ambavyo mifuko ya plastiki inavyoleta athari kwa jamii, mazingira na mifugo pia, wakiiasa jamii kutotumia bidhaa hiyo.
Maonesho hayo yaliwashirikisha wanafunzi takribani 240 wa sekondari na walimu 120 wakionesha kazi mbalimbali za kisayansi.
0 comments: