Kuelekea uchaguzi mkuu wa Raisi, Wabunge na Madiwani utakao fanyika 25/10/ 2015 vyama mbalimbali vya siasa vimeendelea kuchagua viongozi watakao viwakilisha vyama vyao katika ngazi ya Uraisi , wabunge na madiwani
Aliyekua Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa |
Katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam, aliyekuwa Meya wa Ilala, Jerry Silaa amembwaga tena mrufani na mpinzani wake wa karibu Ramesh Patel kwa kupata kura 10, 965 sawa na asilimia 57.1 ya kura zote 19, 187 zilizopigwa.
Sasa Jerry silaa atakiwakilisha Chama Cha Mapinduzi CCM katika nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo la Ukonga.
Baada ya matokeo hayo ndugu Ramesh Patel ambaye alikubali kushindwa na kusaini fomu maalumu za chama hicho amepata kura 6, 960 sawa na asilimia 36.27.
Uchaguzi katika jimbo hilo umefanyika baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoketi mjini Dodoma hivi karibuni kuagiza urudiwe sambamba na majimbo mengine ya Kilolo, Makete na Busega kutokana na dosari kadhaa.
0 comments: