Habari za Magufuli kuahidi kutoa laptop kwa walimu na milioni 50 kwa kila kijiji ikiwa atashinda Uraisi zilienea kwa kasi sana mtandaoni.
Leo Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM alizungumzia suala hilo mbele ya waandishi wa habari na kuonesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM |
Ilani hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.
Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni 50
"Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ".
Amefafanua na kuongeza kuwa "Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi". Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya CCM Ofisi ndogo Lumumba leo.
Ilani ya Uchaguzi CCM 2015-2020 |
0 comments: