Louis van Gaal : Huu utakua Msimu wa Luke Shaw

code         No comments

Luke shaw  beki wa mashetani wekundu Mancherster United atamalizia mfululizo wa mechi za maandalizi za msimu ujao wa ligi kuu England kwa kukipiga na klabu ya PSG ya ufaransa
Luke Shaw (katikati) akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Man U

Show alianza vibaya msimu uliopita wakati kama huu baada ya kuondolewa na Van Gaal baada ya kuonekana kuongezeka uzito sana.

Lakini wakati huu mlinzi huyo mwenye miaka 20 amekua miongoni mwa wachezaji wa mancherster united ambao wanaonesha kiwango kikubwa katika mechi za maandalizi zinazoendelea Marekani.
 
Luke Shaw akigomabia mpira na mcheza wa  Barcelona Sergio Busquets
Van Gaal : “Luke Shaw anakipaji, sio jambo ndogo kutoka Southampton na kujiunga na kablu kubwa kama Mancherster United.
Ingawa anafaida ya kua Muuingereza ukilinganisha na Memphis Depay ambaye ni mjerumani anakutana na tamaduni na mazingira tofauti ya mchezo
Hivyo naamini huu utakua ni msimu wake mzuri zaidi”


 ‘Namwamini na atambue hivyo na nategemea atatuonesha mambo makubwa’

Si kawaida kwa Van Gaal kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kama hivi. Kwa kawaida hupenda kuzungumzia timu kwa ujumla










Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.