Maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dhidi ya Rufaa za Ubunge na Udiwani

code         No comments

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa za Wabunge 55 na imeshatolea maamuzi rufaa 42  bado rufaa za Wabunge 13 ambazo vielelezo vyake vinasubiriwa kutoka kwenye Halmashauri husika. Kulikuwa na Rufaa 16 za Wabunge waliokuwa wameenguliwa. Kati ya hizo Wabunge 13 wamerudishwa kuendelea na kampeni na rufaa 3 Tume ilikubaliana na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi hivyo hao hawatarudishwa kwenye orodha ya Wagombea. Aidha, rufaa 24 zimekataliwa na Tume ambapo maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yataendelea kubaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea. Pia kuna rufaa 2 ambazo Tume haijazijadili kwa kuwa hazikufuata utaratibu wa kuwasilisha Tume yaani kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo husika hivyo, maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yatabaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea kama walivyoteuliwa. 

2.   Rufaa za Madiwani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa za Madiwani 200 na imeshatolea maamuzi rufaa 82  bado rufaa za Madiwani 118 ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi. Kulikuwa na Rufaa 16 za Madiwani waliokuwa wameenguliwa. Kati ya hizo Wabunge 15 wamerudishwa kuendelea na kampeni na rufaa 1 Tume ilikubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi hivyo hao hatarudishwa kwenye orodha ya Wagombea. Aidha, rufaa 64 Tume ilikubaliana na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi hivyo yataendelea kubaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea.


Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.