Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikusanyiko ya Kampeni ya Rais. Mikusanyiko hiyo yenye sura ya Kampeni haipo katika Ratiba ya Kampeni ya Urais.
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi |
Mikusanyiko hiyo yenye sura ya kampeni inaweza kuingiliana na ratiba za kampeni za chama kingine katika maeneo husika na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani.
Iwapo Chama cha Siasa kinachotaka kufanya mikusanyiko yenye sura ya Kampeni za Uchaguzi kinapaswa kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ili aweze kuitisha Kamati ya Ratiba ya Kampeni ya Rais inayojumuisha vyama vyenye Wagombea wa Kiti cha Rais ambavyo kwa mujibu wa kanuni tajwa hapo juu, vinaweza kukubali au kukataa mapendekezo hayo.
Vyama vyote vya Siasa vizingatie Ratiba ya Kampeni ya Uchaguzi wa Rais na viache kufanya mikusanyiko ya aina yoyote ambayo haipo katika Ratiba ya Kampeni ya Rais.
Chama kitakachokiuka maelezo haya kitakuwa kimekiuka kipengele cha 2.1. (a) cha Maadili ambacho kinaelekeza kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa na Wagombea kuheshimu na kutekeleza Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uchaguzi, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Sheria zingine za nchi katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi adhabu zake zimefafanuliwa katika kipengele cha 5.10 na 5.12 cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.
0 comments: