Mgombea Ubunge wa wa chama cha wananchi CUF jimbo jipya la nanyamba wilaya ya mtwara vijijini, Twahiri Saidi amebomolewa nyumba yake na wananchi wenye hasira kali kufuatia kushindwa kurudisha fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku akizima simu.
Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachi wa jimbo la Nanyamba wamesema mazingira aliyotoweka mgombea huyo yanaonyesha wazi kuna mchezo mchafu umefanywa ili kutoa fursa kwa mgombea wa CCM Abdallah Chikota kupita bila kupingwa.
Naye katibu kata wa CUF kata ya Milango Minne eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo.
Jeshi la Polisi mkoani humo limewataka wananchi kuwataja walio bomoa nyumba hiyo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo wake.
0 comments: