Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtangaza Edward Lowassa kuwa ndie mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwezi Oktoba mwaka huu.
Lowassa, ambaye ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, amejiunga na Chadema wiki moja tu iliyopita akitoka chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka thelathini. Kwa uteuzi huo,
Lowassa atapambana na mgombea urais wa CCM John Magufuli ambapo wote wanaelezwa kuwa na wafuasi wengi. Mwandishi wetu mjini Dar es Salaam ametuandalia taarifa hii
0 comments: