Kipindupindu Chaendelea Kutesa Dar na Moro : wagonjwa 262 Waripotiwa , 8 Wafariki

code         No comments

Idadi ya wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao umelikumba jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia wagonjwa 262,huku vifo hadi sasa toka ugonjwa huo ugundulike Agost 15 mwaka huu vikifikia nane.
mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif Rashidi wakati akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa taarifa juu ya Ugonjwa huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani Morogoro.

Aidha alisema kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam walioambukizwa ni 230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya Kinondoni ina wagonjwa 186,Manispaa ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba wagonjwa waliyolazwa kwenye kambi za matibabu ni 71 ambazo ni Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15 huku kambi ya Temeke ni wagonjwa 9.

Aliendelea kufafanua kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakitoka katika maeneo mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni maeneo ya Makumbusho, Kimara, Tandale, Manzese, Saranga, Magomeni, Mwananyamala, Kibamba, Kigogo, Goba, Mburahati, Kinondoni na Kijitonyama.

Manispaa ya Ilala ni Buguruni,Majohe, Chanika, Ilala sharif shambana Tabata huku Katika Manispaa ya Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa Azizi Ally, Keko na Yombo Vituka.

Alisema Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15 wamehifadhiwa kwenye kambi ya Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.

Waziri huyo wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua tahdhari pamoja na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa mazingira,kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula chakula, kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo vimeandaliwa kwenye mazingira safi na salama.

Naye mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora amesema kuwa lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa kemikali maalumu na kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji au kuchemsha maji.

Aidha aliongeza kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti kushugulikia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazigira katika maeneo husika nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya pekee bali ni ushirikiano na Wadau wengine ikiwemo sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, Maji na Elimu.

Katika hatua nyingine Wizara ya Afya imetoa namba za simu ya mkononi kwa wananchi ambazo ni 0767300234 ambapo zitatumika kuwasiliana moja kwa moja na mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili kupata maelekezo ya kitabibu mara baada ya kuhisi dalili za maambuki ya ugonjwa huo.

Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.