Bale Atamani namba nyingine Real Madrid

code         No comments


Bale alicheza fowadi wa kati juzi Jumanne kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu yake ya zamani ya Tottenham Hotspur na kufunga bao katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Real Madrid kushinda 2-0.

SUPASTAA wa Real Madrid, Gareth Bale amesema atapenda zaidi kama atacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati msimu huu.

Kwenye mchezo huo, kocha Rafa Benitez, alimtumia Bale pia kama namba 10 mahali ambako alionyesha uwezo mkubwa.
Real Madrid ina nyota wengi wa kucheza eneo hilo akiwamo Isco na James Rodriguez, lakini Bale anaamini ni mahali pazuri kwake kuonyesha kiwango na kipaji chake cha soka.

“Hii ndiyo nafasi yangu bora zaidi. Nilipokuwa Tottenham, nahisi nilikuwa nikicheza soka langu bora, kwa sababu nilicheza kwenye nafasi hiyo, kwangu nadhani ni nafasi nzuri zaidi,” alisema.
“Mahali hapo nakuwa na uwezo wa kwenda kushoto na kulia kitu ambacho nilikuwa nakifanya Tottenham na hivyo pia nikiwa na Wales. Ni jambo zuri kuwa na sapoti kutoka kwa kocha na rais (Florentino Perez), nitawalipa mabao na mataji.”

Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.