JK aeleza sababu za CCM kumsimamisha Dk. Magufuli

code         No comments

 Rais Jakaya Kikwete amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha, Dk. John Magufuli (pichani), kugombea urais kupitia chama hicho kwa kumuamini kuwa atasimamia vizuri rasilimali za nchi ikiwamo gesi na madini kwa manufaa ya taifa na Watanzania.



Akizungumza jijini Arusha juzi wakati akifungua mkutano wa nne kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-Tamisemi), Bodi ya Mfuko wa Barabara na wadau wa barabara, Rais Kikwete alisema ana amini endapo Magufuli atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania waKati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, atasimamia vizuri rasilimali hizo kutokana na kuwa msomi mzuri na kuwa na uchungu wa maendeleo ya taifa lake na watu wake.

“Huyu Magufuli siwezi kujilinganisha naye, mwenzangu ana PhD ya kusomea na ameifanyia utafiti kwenye ganda la korosho jinsi ya kutumia mafuta yake kunufaisha nchi kwenye maendeleo ya taifa, ila mimi nina PhD ya heshima, hatuwezikuwa sawa, hivyo nina imani naye sana,” alisema.

Rais Kikwete alisema CCM imemchagua kwa makusudi Dk. Magufuli kwa ajili ya kuhakikisha nchi inaneemeka na rasilimali ya gesi ambayo hadi sasa uwekezaji wake umegharimu dola za Marekani bilioni 20 hadi 30 mpaka kuanza uvunaji wake.

“Naomba tusifanye mchezo na rasilimali hii, ndiyo sababu  mimi nimehakikisha tunakuwa na sheria nzuri ya kusimamia vizuri rasilimali hii isije ikatupeleka kubaya, japo baadhi ya watu walisema naharakisha ya nini, ila najua kuna nchi walipata mafuta ila watu wakubwa wakakopa kwa kujivunia mafuta hayo na matokeo yake hadi sasa wanalipa madeni na nchi, mimi sikutaka hayo,” alisema.

Alisema ni vizuri rasilimali kama hizo zikawekewa utaratibu wa kuzilinda kabla ya kuanza uvunaji wake na kwamba baada ya miaka michache ana amini Tanzania itakuwa nchi tajiri kwa kuuza gesi nje kwenye masoko makubwa.

Rais Kikwete alisema Dk. Magufuli kutokana na usomi na uchapakazi wake, kila wizara aliyowekwa aliongoza vizuri na kupatikana mafanikio makubwa, hivyo akiwa Rais atafanya mambo mengi makubwa zaidi kwa manufaa ya taifa na wananchi wote


Published by code

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Si vous n'avez pas eu la chance de prendre dans tous.
Follow us Google+.

0 comments:

© 2014 punguzo . Designed by Bloggertheme9
Powered by Blogger.