Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,Makao Makuu ya CCM,Ofisi Ndogo Lumumba.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa leo Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaa chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imefanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia.
Wagombea Ubunge walioteuliwa na majimbo yao kwenye mabano ni:-
Ndugu Jerry Slaa - (Ukonga) Dar es Salaam
Ndugu Edward Mwalongo - (Njombe Kusini) Njombe
Ndugu Venance Mwamoto - (Kilolo) Iringa
Ndugu Raphael Chegeni - (Busega) Simiyu
Ndugu Edwin Ngonyani - (Namtumbo) Ruvuma
Ndugu Mohamed Mchengerwa - (Rufiji) Pwani
Ndugu Norman Sigara - (Makete) Njombe
Ndugu Martin Msuha - (Mbinga Vijijini) Ruvuma
Ndugu Joel Makanyanga Mwaka - (Chilonwa) Dodoma
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/08/2015
0 comments: